Saturday, January 5, 2013

NINI MAANA YA MAPENZI


MAPENZI

Kila binadamu hupenda jambo fulani. Mapenzi ya mtu juu ya jambo yaweza kumvutia kiasi kwamba anaweza kupoteza welekeo wa maisha yake. Watu hupenda hadi kileleni. Hapa ndipo mtu aelewi hili wala lile. Hali hii si tu kwa vijana wanaoingia katika umri wa balehe bali hata kwa wale waliovuka umri huu. Kweli kila mtu anahaki ya kupenda. Na mapenzi haya yalianza pale binadamu walipoanza kuishi pamoja kama mke na mume kama vitabu vyetu vya dini vinavyoelekeza, ambavyo ni Biblia na Kuruhani.

Napenda kuwa muwazi sana juu ya aina ya penzi ninalozungumzia. Ni yale mahusiano ya kimwili yaliyopo kati mwanamke na mwanaume. Haya ndiyo mahusiano ninayozungumzia na sizungumzii yale ya watu wa jinsia moja. Mapenzi hayauzwi na ayachagui rangi wala kabila.Mapenzi ni kitu asilia ambacho  humkuta mtu juu ya mtu mwingine ambaye anaweza kuwa mwanamke kwa mwanaume au kinyume chake. Na hawa kila mmoja hutokea kumpenda mwenzake mpaka kufikia kilele cha penzi.

Angalia mfano huu; umepita wapi na kutembea mikoa mbalimbali au wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa mingapi? Umekutana na wangapi wazuri (wanawake au wanaume), na ulimpenda yupi. Inawezekana kati ya uliowachagua hakuna hata mmoja kati ya wale uliokutana nao ukaridhia kuwa naye. Lakini ulikutana na kijana mmoja ambaye amekuvutia sana zaidi ya asana na mahusiano ukaanza kuanzisha mpaka leo ni mke wako au mchumba wako. Hapo ndipo ninaposema “love is something natural” na si kitu cha kubahatisha tu.

Na ieleweke kwamba mke mzuri ni wako tu, na mme mzuri ni wako tu. Hakuna ubishi kwa hili. Na pale unapoona kuwa mke au mme wako si mzuri basi ulikosea wakati wa uchaguzi  wako. Hapo huna budi kuonyesha unampenda kama kitabu hiki kinavyoeleza uk.6 & 7. Na ujue kwamba kila mtu ana haki ya kupendwa na mme, mke au mchumba wake. Penye upendo pana mapenzi ya kweli.

NINI MAANA YA MAPENZI?

Neno mapenzi ni pana sana. Na kila mtu huweza kufikiri kulingana na uelewa wake juu ya mapenzi kati ya mtu na mtu. Mapenzi ni ile hali asilia ambayo mtu anakuwanayo kwa mtu mwingine na inapaswa kuwa na makubaliano baina ya wahusika ambayo yaweza kuwa ya muda mfupi au muda mrefu. Wengine husema mapenzi ni ile hali ya mtu kuwa na mahusiano ya kimwili  na mwingine.

Kipindi tulichopo sasa ni kipindi cha utandawazi. Si mtoto mdogo si wakubwa wote wanayafahamu mapenzi yalivyo. Kwa sasa imekuwa kawaida kwa kila mtu kuanza uhusiano hata kabla ya kufunga ndoa. Hii ndiyo ninayoita utandawazi. Watoto wadogo hupata habari hizi kupitia masimulizi kutoka kwa kaka na dada zao nyumbani au nje. Hii haikuwa tamaduni yetu, lakini sasa ni jambo la kawaida kwa mwanafunzi wa darasa la tano kukutwa na ujauzito. Lakini ni kwa mazingira hayahaya.

Kipindi hiki ndicho kipindi kigumu kwa vijana kujua yupi ni mke/mme mwema na yupi si mke/mme mwema. Athari hizi huwakuta sana akina dada ambao wakizidisha miaka ishirini na saba, yule ambaye alikuwa mme mzuri anampoteza ndani ya miaka 18 hadi miaka ishirini. Ndani ya miaka hii mwanamke huvutia na anaonekana kama ua linalovutia wadudu (Dr Isack Ndodi, 2011). Nakubaliana sana na maneno ya Dr. Ndodi akizunguma Channel 5 kati ya mwezi Mai hadi Juni, 2011.

Kuna ukweli uliopo juu ya hili. Ndani ya miaka hii mwanamke ujikuta anaingia katika majaribu yasiyo na msingi huku akijitahidi kutafuta mme mzuri kwake, na matokeo yake huishia kuchezewa na hatimae kukosa wote. Wanaume ndio wasababishaji wakubwa wa mke huyu asiolewe au asipendwe. Angalia mfano huu, mti ukichipuza maua utamuona mdudu wa kila aina akiwemo nyuki, nzi, kipepeo na wengine wemgi wakiingia na kutoka. Haya ndiyo yaliyopo kwa wanawake kwa kipindi hicho tajwa hapo juu.

Hapa lile neno langu love is something natural (mapenzi ni kitu cha asili) hutumiwa vibaya na badala yake mapenzi hupoteza umaana wake. Kwa kila mtu mwenye upendo wa kweli hawezi kumdarau mchumba au mke/mme wake. Na inapotokea vinginevyo ni makosa ya kibinadamu ambayo hutokea baina ya hawa wapendanao.

 



No comments:

Post a Comment