Saturday, January 5, 2013

NAMNA YA KUTATUA NA KUEPUKANA NA MAMBO YAWEZAYO KUSABABISHA KUTENGANA


NAMNA YA KUTATUA NA KUEPUKANA NA MAMBO YAWEZAYO KUSABABISHA KUTENGANA

Kufanya uchaguzi sahihi wa mchumba. Kila mtu anashauriwa kuchagua mchumba anayekufaa. Si kila mwanamke au mwanaume ni mzuri kwako na kuanza maisha kama wanandoa. Jaribu kutafakari na kupata ushauri wa watu walio karibu naye ili upate juu ya tabia aliyonayo. Ukiona ni mzuri unaweza kuanza hatua za kufunga harusi.
Si vizuri kuparamia mwanaume au mwanamke unayekutana kwenye basi au kwenye mitandao ya kijamii kama facebook. Kweli watu wanamaneno matamu na mazuri sana, lakini walio wengi ni wababaishaji wa mapenzi. Jiulize swali dogo tu, ameonana na wanaume au wanawake kama wewe wangapi. Jibu ni wengi, hivyo kuwa mtulivu, siku ikiwadia utampata mzuri zaidi ya huyo (simahanishi mtengane na mme/mke au mchumba uliyenaye sasa).

Wazazi hawana budi kupewa elimu ya kutosha juu ya mke/mme au mchumba wako. Mwenye haki ya kuchagua mchumba ni wewe na sio wazazi wako. Wewe ndiye unayefahamu unampenda kiasi gani. Jaribu kuwashauri hadi wakuelewe kwa nini unataka kuwa na huyo mchumba wako. Hapa hauna budi kupunguza hasira kwani wazazi wengine wana tabia ile ya kuhukumu mtu mara tu baada ya kuanza kuongea naye.
Kama wapendanao hamna budi kuendelea kushirikiana nao kwa karibu, na mwisho wa siku hali waliyonayo itatoweka na badala yake uhusiano wenu utaendelea kukua. Usiwatamkie maneno makali wale wote wanaokupinga juu huyo mchumba wako. Kwa kufanya hivyo uhusiano wenu utadumu maisha milele.

Ni muhimu kuweka makubaliano juu ya dini za wapendanao. Hili ni jambo linaloumiza sana vichwa vya watu ulimwenguni. Suala hili ni suala la mdahalo usio na mwisho, na uhishia tu pale wapendanao wanapoamua kufuata majibu na mapatano yao.Kama mke/mme wako ni dini tofauti na yako, basi nakushauri muanze kupanga mikakati pale tu mutapoamua kuanza uhusiano wenu. Mweleze ukweli huyo mchumba wako juu ya dini yenu na mnavyoishi kule kwenu. Baada ya hilo muendelee kupanga hatima ya kizazi chenu na athari zipi zitawapata na mutatatua vipi hizo changamoto zote. Changamoto ambazo huathiri sana ni hatima ya watoto. Hapa kama msimamo haupo juu ya maamuzi yenu basi tambueni huo utakuwa mgogoro usio na mwisho. (Hapa nimezungumzia tu kwa wale walio na wanaotarajia kuingia kwenye uchumba).
Kwa wanandoa kama walifanya maamuzi bila kujijua basi nashauri waendelee kufuata utaratibu wao na pale inaposhindikana muwaone wataalamu wa masuala ya mahusiano katika jamii wakiwemo watu wa ustawi wa jamii.

Ni vizuri kumfikisha mwenza wako kileleni. Wanaume walio wengi hushindwa kuwafikisha wake zao kileleni. Hii yote inatokana na kushindwa kujua namna gani ya kumwandaa mke au mchumba wake ili afikie kileleni. Walio wengi wanaamini wakishafikia hatua ya kupezi mara mbili wanaona wamemfikisha mke kileleni. Nakushauri usome kitabu kilichoandikwa na Dr Paul. Mara nyingi husikika siku ya jumatano katika RFA (Radio Free Africa) kuanzia saa tano usiku.
Utajua namna ya kumfikisha mke wako au mme wako kileleni. Pia kuna wanaume ambao hukosa kufikia kileleni. Hii husababishwa na mke kutojua namna ya kumfikisha mme kileleni. Hivyo kupitia kitabu cha Dr Paul Nelson utaweza kujua sehemu zipi zinapaswa kuguswa ili kumfikisha kileleni. Kitabu kinachozungumzia namna ya kumfikisha mpenzi wako kinaandaliwa. Kwa wale wapenzi wa facebook munaweza kutembelea ukrasa wangu wa facebook au Arasachi The Centre of Learning”
Kikiwa tayari muda wowote utakiona sokoni. Kitakuja na kichwa cha habari kisemacho “unafahamu namna ya kumwandaa mpenzi wako?”. Kulingana na mwili wa mwanamke ulivyo, unaweza kufanya tendo la ndoa hata masaa mawili na asifikie kileleni. Mke au mme akifanya vizuri juu ya hili hawezi kumtamani mme au mke mwingine kwa sababu utakuwa umemjenga kisaikolojia.

Ni vizuri kujizuia tabia ya umalaya kabla na baada ya kuanzisha uchumba. Hakuna mwenza anayependa kuona mke/mme wake anatabia ya umalaya. Wengi huzaliwa nayo na kurithi kutoka kwa wazazi. Na wengine hujengwa na makundi mchanganyiko katika jamii zikiwemo taasisi za kufundishia.
Kwa mfano Vyuo vikuu nchini Kenya au nchi za Magharibi ni kawaida kuwaona wanafunzi wakishikana sehemu mbalimbali za miili yao wakiwa maeneo tofauti tofauti ya shule au chuo chao (hawa ni wanalika “peer group”).
Muhusika hauna budi kujizuia kwa kuwa naye karibu yule mpenzi wako. Na inavyotokea unaishi naye mbali basi mtembeleane wakati wa likizo na kupata muda wa kuongea pamoja. Pia jiepushe kwenda maeneo ya starehe kama vile baa na ufukweni ukiwa pekeyako pindi mpenzi wako yuko mbali nawe. Kwa kufanya hili tabia yako  utakuwa umeizuia na kuiacha kabisa.

Mawasiliano lazima yadumishwe. Mwanzo wa penzi mawasiliano huwa ni ya hali ya juu kwa sababu kila mmoja anapenda amjue vizuri mpenzi wake. Hii yote hutokea kwa sababu ya upendo walionao kwa kila mmoja kwa mwenza wake. Siku zinavyosonga mawasiliano huanza kufifia au kuongezeka kutegemeana na lugha inayoyumika. Hali ya kufifia mara nyingu hutokea tu mara baada ya kuanza zoezi zima la mapenzi kwa siku ya kwanza.  Baadhi ya wanaume hukosa hamu ya kuendelea kuwa naye kama mpenzi wake. Lakini baada ya siku chache mkizidi kuwasiliana hali inarudi kama kawaida. Hii hutokea sana kwa wanaume, na kama kwa wanawake ni kwa kiasi kidogo sana. Hapa ndipo utapoona yule uliyempenda umetengana ghafla.
Mukifikia hatua hii mnapaswa kuendeleza na mawasiliano. Kwani kitendo cha kutengana ghafla huwaumiza sana wanawake kwa sababu inaonekana lengo kubwa ni kumchezea na kumwacha. Ili kudhibiti hali hii mnatakiwa kudumisha mawasiliano na kuendelea kuwa karibu sana na baada ya wiki moja hali itarudi na kuwa na hamu ya kuwa na wewe muda wote. Hapo ujue kuwa hali imeshatoweka na sehemu iliyobaki ni ya kuendelea kujipangia mikakati juu ya mahusiano yenu ili kudumisha penzi lenu. (hali hii ni kwa baadhi tu ya watu na hutokea kama mke au mme hakuweza kumfikisha kileleni mwenza wake. Ni vizuri mfanyie surprise ya ukweli siku ya kwanza ili asikusahau kamwe maishani mwake. Walio wengi huikumbuka sana yale yaliyotendeka siku ya kwanza kufungua penzi lao).



No comments:

Post a Comment