Saturday, January 5, 2013

ATHARI ZA KUPENDA KUPITA KIASI


ATHARI ZA KUPENDA KUPITA KIASI
Ni vyema kujua mpenzi wako anakupenda kiasi gani. Na kila mtu ni siri yake mwenyewe kujua anampenda mwenzi wake kwa kiasi gani. Kumpenda mke au mme au mchumba wako ni jambo jema sana. Muonyesheshe namna upendavyo kwa maneno, pamoja na tabia yako.

Kuna jambo moja ambalo mtu yeyote apendezwi nalo kuona mme, mke au mchumba akilitenda ambalo ni kuonyesha dharau ikiwemo kuona maneno anayozungumza hayana mantiki yeyote. Akigundua mwezi wako ujue kuwa hali ya penzi lenu  linaelekea kubaya. Si vizuri kuendekeza hali hii kama umezaliwa nayo au kurithi kutoka kwa wazazi. Inapaswa ujizuie.

Hakuna mapenzi ya kweli kama hakuna upendo. Katika maisha ya sasa ni muhimu sana kuonyesha namna unavyompenda mke/mme wako. Watu hupenda sana kiasi kwamba hata kufikiri suala lingine, badala yake huitaji kukaa muda wote na kumfuata kila aendako. Na wengine ufikia mahali hadi anaharibu kazi. Kila kazi anafanya ili mradi aonekane amefanya kazi.

Kwa kawaida imezoeleka kuona mke au mwanamke ndiyo anayependa sana kuliko mme wake. Kiukweli ni kwamba wote wana haki ya kuonyesha kila aina ya upendo alionao kwa mweza wake.

Zifuatazo ni athari za kupenda kupita kiasi kwa wapenzi:-
-Kushindwa kutekeleza majukumu ya kila siku ikiwemo ya kiofisi kwa wafanyakazi.
-Siku ya kutendwa ikiwadia basi kwa aliyetendwa ni rahisi kupata mshtuko wa moyo (stress) au kujiua.
-Kutosalimiana kwa muda mrefu.
-Kushindwa kusaidiana kwa namna moja au nyingine hasa yale yaliyo nje ya mpaka.


Nadhani umejifunza mengi sana katika kitabu hiki. Ni jukumu lako kubadilika na kuwa katika mstari mnyoofu. Mpende mke/mme au mchumba wako lakini usipitilize kiwango kiasi kwamba unapoteza welekeo wa maisha yako. Utaumia na kushindwa kufanya maamuzi yako kwa wakati husika.

No comments:

Post a Comment