Saturday, January 5, 2013

MAMBO MAKUU YANAYOSABABISHA KUTENGANA KWA WAPENDANAO


MAMBO MAKUU YANAYOSABABISHA KUTENGANA KWA WAPENDANAO

  1. Kutofanya uchaguzi ulio sahii wa mke/mme au mchumba. Vijana wengi siku hizi hujilaumu sana  juu ya chaguo la mwenza wake. Ukikosea mwanzo ujue utaoa na kuacha mke zaidi ya mmoja. Pakifikia mahali unaanza kutamani wanawake/mwanaume wa nje na kumsahau wako wa ndani ujue ni ishara kwamba hukufanya chaguo zuri ujana wako.
  2. Wazazi kutopendezwa na mke/mme. Hapa wazazi nawazungumzia wale wanaopenda kuingilia mambo ya ndani ya watoto wao. Kuna watu wanaitwa mawifi, hawa ndio chokochoko kubwa na mke na mme kutengana. Watatumia maneno ya uzushi na unafiki ili mradi mke au mme yule waachane. Mwisho ndoa au uchumba unavunjika.
  3. Dini tofauti. Hili ni suala la mdahalo karibu dunia mzima. Inapotokea mme na mke wameanzisha uchumba, na kila mtu ana dini yake, mwanzo wa penzi hakuna aneyekumbuka nini athali kwa hapo baadaye. Muda unasonga, na kila mmoja anahitaji afunge ndoa au wazazi wafahamu, hapa kila mmoja anaanza kukumbuka utofauti wao. Kutokana na imani kali au kutokuwa na uelewa mwanzo, wanaamua kutengana ili kulinda maslahi ya dini au dhehebu la kila mtu. Hii mara nyingi hutokea kama mmoja wao ni Mkristo au Muislam. Katika ndani ya ukristo kuna misingi inayoongoza kanisa la SABATO. Hapa pia hawaruhusu muumini kuoa au kuolewa nje ya dhehebu hili   vinginevyo anatengwa na kanisa.
  4. kutofikia kilele wakati wa tendo la ndoa. Hakuna ndoa inayoweza kudumu kama tendo la ndoa halifanyiki. Au kama linafanyika ni kwa kulidhika mmoja na mwingine asitosheke. Hii ni sahemu muhimu sana inayomfanya mke au mme aweze kuwa na mahusino na mtu mwingine ili aweze kujitosheleza. Kila mmoja hupenda atosheke, na inapotokea vinginevyo migogoro huanzia hapo na hatimae kuvunjika kwa penzi lao. Zao la hili ni kutoroka kwa mke/mme au mchumba na kuanzisha uhusiano na mtu mwingine.
  5. Tabia ya uzinzi kupindukia. Hapa nazungumzia tabia ya umalaya ya mwanamke au mwanaume nje ya mpenzi wake. Hawa ni watu ambao uzaliwa na genes za aina hiyo na wamerithi kutooka kwa wazazi. Hivyo kwa mtu aliyorithi inakuwa ni rahisi zaidi kutoka nje ya ndoa yake na kwenda kufuata wengine ili mradi atimize malengo yake. NB. Tumetoa njia za kutatua hili katika kitabu hiki.
  6. Maneno au mawasiliano. Namna mke na mme wanavyozidisha mawasiliano, ndivyo wanovyoongeza penzi lao. Kwa zamani barua zilikuwa ndio chombo cha mawasiliano kama mmoja wao aliishi mbali. Lakini kwa sasa ni njia ya simu za mkononi. Inapotekea mawasiliano yanapungua kati ya mme na mke kinachofuata ni kusauliana. Kila mmoja atapata wazo la kuwa na mwingine na hatimaye kuanzisha mahusiano mapya na yule ambaye hakupenda kuwa naye. Usipokuwa makini juu ya hili lazima mutatengana tu.
  7. Wivu. Hakuna penzi linaloweza kudumu kama hakuna wivu. Na wivu huo uwe wa kiasi ambacho akiwezi kuathili penzi lao. Kuna watu wana wivu kupindikia. Hili ni tatizo kubwa, na hakuna mtu anayependa afanyiwe wivu kiasi kwamba hadi mtu anakosa uhuru. Pakifikia mahali hapa wapendanao huanza kutoa maneno ya siri kwa jirani na mwishowe kutengana kwa wependanao. Hapa pia inaambatana na hali ya kutokuwa na imani na mwenza wako.
  8. Kuwa na mahusiano ya hali ya juu na mtu wa jinsia tofauti pamoja na utani. Mtu ukishaolewa, kuoa au kuwa mchumba ni bora zaidi upunguze mahusiaona ya kupindukia na watu wa jinsia nyingine. Hali ya utani unaoambatana na kushikana, kubusiana pamoja na kuelezana maneno ya kimapenzi kwa wale ambao si wapenzi wako husababisha mgogoro na mwenza wako. Vinginevyo ndoa au uchumba ule utaelekea mahali pabaya na mwisho kuvunjika kwa penzi.
  9. Kusikiliza maneno ya watu. Kuna watu hupenda kuchonganisha wanawake au wanaume wa watu kwa maslai binafsi. Kwa kawaida watu hawa wapo kwa ajili ya kuona mnagombana. Hivyo basi, kusikiliza kwa maneno ya hawa watu inapelekea kubadili kwa mwenendo wa mweza na hatimaye kuwa mwisho wa penzi.
  10. Ugumba/tasa. Hii ni ile hali ya mmoja kati ya wapendanao kutokuwa na uwezo wa kuzaa. Yaani kwa mwanaume kushindwa kutoa mbegu zinazoweza kusababisha kutungwa kwa mamba, na kwa mwanamke kushindwa pia kutoa mayai yenye uwezo wa kupokea mamba. Hali hii huwaathiri sana wanawake ambapo mke huonekana mzigo mzito katika nyumba. Wangine wanafikia mahali wanawaambia wapenzi wao kuwa wanajaza choo tu. Hii kauli lazima ipigwe vita sana. Madhara ya kauli zinazofanana na hizo, yule mwenye kizazi huamua kumwacha yule asiye na kizazi na kwenda kufungua kizazi kipya na mtu mwingine.

Hizo ni baadhi ya sababu za kimsingi zinazochangia uvunjifu wa ndoa au uchumba. Ukweli ni kwamba sababu zipo nyingi lakini zinazoumiza sana vichwa vya watu ni hizi.Hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini juu ya mambo haya yaletayo mzozo katika penzi husika.


No comments:

Post a Comment